KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel leo imetangaza washiriki walioingia tano bora ya shindano la kusaka na kuibua vipaji vya wanamuziki chipukizi la Airtel Trace Music Star.
Shindano hilo lililozinduliwa rasmi Oktoba mwaka jana, sasa limefikia hatua ya fainali ambapo mshindi wa Airtel Trace Tanzania atapatikana katika fainali inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Februali mwaka huu.
Mshindi atapata fursa ya kwenda kushiriki mashindano ya Airtel Trace Music Award Afrika, yatakayoshirikisha washiriki wengine kutoka nchi 13 barani Afrika.
(HABARI/PICHA: DEOGRATIUS MONGELA NA DENIS MTIMA/GPL)