Airtel kupitia huduma ya Airtel Money yazindua huduma mpya ya kufanya malipo kwa kutumia kadi nchini
· Airtel yaja na Huduma mpya sokoni ya malipo ya kadi kwa kupitia huduma ya Airtel Money Near Field Communication (NFC)
· Airtel yalete Huduma ya kulipa kwa kugusisha kadi ya Airtel Money kwa mara ya kwanza nchini
· Wateja na wafanyabiashara wawezeshwa kufanya miamala kirahisi zaidi kwa kugusisha kadi ya Airtel Money
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo (mwishoni mwa wiki) imetangaza huduma ya kwanza sokoni inayotumia kadi maalumu kwa kupitia huduma ya Airtel Money. Huduma hiyo mpya inayowawezesha wateja wa Airtel Money kufanya malipo kwa kutumia kadi imeanza katika mkoa wa Arusha na itaendelea kufikishwa katika mikoa mbalimbali nchini
Akiongea kuhusu huduma hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Aijaza Khan alisema” technologia inakuwa kwa kasi na tumeonelea ni muhimu kwenda sambamba na mabadiliko hayo kwa kuleta huduma za kibunifu zitakazokithi mahitaji ya wateja wetu yanayokuwa kwa kasi kila siku. Nia yetu ni kuona wateja wetu wanapata huduma za kisasa kwa wakati wote. Huduma hii mpya tunayoitambulisha leo itawawezesha wauzaji na wanunuzi kupata njia rahisi, ya uhakika na salama ya kufanya miamala na malipo yao ya kila siku. ili kutumia huduma hii kila mteja atatakiwa kupata kadi maalum inayomuwezesha kufanya malipo kirahisi , kwa haraka na kwa usalama katika maduka mbalimbali yaliyopatiwa vifaa maalumu kwaajili ya kupokea malipo toka kwa wateja. Huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wafanyabiashara na wateja wetu Arusha.
“Kadi hii maalumu imeunganishwa na akaunti ya Airtel Money ya mteja, mteja anachotakiwa ni kugusisha kadi yake na kifaa cha kupokea malipo (POS) ili kuweza kufanya malipo. Malipo yatakamilika pale mteja atakapothibitisha muamala kwa kuweka namba yake ya siri kwenye kifaa cha malipo
Tunajivunia kuwa mtandao wa kwanza Tanzania kuanzisha huduma hii ya kibunifu itakayowawezesha wateja wetu kufanya malipo ya kwa urahisi, haraka , kiusalama bila kuwa na haja ya kupiga namba ya Airtel money na kuingia kwenye orodha, Kwa kutumia kadi maalumu mteja anaweza sasa kufanya malipo. ”. aliongeza Khan
Akiongea kuhusu faida za huduma hiyo , Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” huduma hii inafaida nyingi kwa wafanyabishara na wateja ikiwa ni pamoja na njia salama ya kuifadhi pesa, ya kuhakiki na kukusanya pesa,mfanyabiashara anaweza kuzipeleka moja kwa moja benki kutoka kwenye kifaa hicho au kutoa pesa kwa wakala aliye karibu. Kwa upande wa wateja faida hizo ni pamoja na kufurahia urahisi, usalama, uharaka wa kufanya malipo na pia kuepusha wateja kutembea na pesa nyingi mfukoni ili kufanya malipo. Mteja atakapopoteza au kuibiwa kadi yake pesa zake kwenye kadi yake zinabaki salama aliongeza” Matinde
Akiongelea kuhusu uzoefu alioupata a kutumia huduma hii ya kadi kupitia Airtel Money, Mfanyabiashara na milliki wa Phamarcy Bi Elizabeth Mshana alisema” Huduma hii ni ya kipekee na imerahisisha sana namna ya kufanya biashara maana ni rahisi kutumia na ni salama. Wateja wanapokuja dukani kununua dawa na hawana pesa taslimu mfukoni wanatumia huduma hii na mimi kama muuzaji nafurahi kwakuwa pesa zangu ziko salama na sina haja ya kufikiri kuhusu kutafuta chenji. Kwa kweli ni huduma nzuri na tunaifurahia na nawashauri wafanyabiashara wenzangu na wateja kutumia huduma hii kwani inaleta ufanisi”
Huduma hii inapatikana sehemu mbalimbali ikiwemo maduka ya biadhaa , maduka ya chakula, maduka ya dawa, mawakala wa Airtel Money na Baa, Mpango mkakati ni kufikisha huduma hii katika maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka huu.
Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money hivi karibuni imezindua huduma nyingine ya kibunifu ijulikanayo kama Timiza inayowawezesha wateja wake kupata mikopo rahisi papokwa papo na kurejesha baada ya wiki moja au mwenzi huduma ambayo imewawezesha watanzania wengi kuboresha mitaji ya biashara zao na kutatua changamoto ndogondogo za kila siku
Na GSENGO BLOG