Wanajeshi wa serikali waliokuwa wakipiga doria katika mji wa Baga kabla ya Boko haram kuuteka pamoja na kambi ya kijeshi
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa kundi la Boko Haram limeuteka mji na kambi moja ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa kimataifa wanaojaribu kukabiliana na wapiganaji hao.
Seneta wa Borno Kazkazini Maina Ma'aji Lawan,eneo la mji wa Baga amesema kuwa wanajeshi waliitoroka kambi yao baada ya kushambuliwa na Boko Haram jumamosi asubuhi.
Wakaazi wa Baga,ambao walitoroka kupitia maboti hadi taifa jirani la Chad,amesema kuwa raia wengi wameuawa na mji huo kuchomwa.
Wapiganaji wa Boko Haram tayari wanadhibiti eneo kubwa karibu na mji wa Baga,ambao hadi kufikia jumamosi ni miongoni mwa miji michache iliokuwa imesalia na serikali.