Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Mfanyakazi wa kivuko cha Kigongo -busisi mkoani Mwanza akionesha wananchi namna ya kutumia mashine hiyo.
Na JOHN DOTTO, Mwanza .
WAZIRI
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ameagiza kufungwa kwa mfumo mpya wa
kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja
wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo.
Mbali
ya hilo, ameagiza kufanywa kwa utaratibu utakaowezesha huduma katika
vivuko zinatolewa kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Dkt.
Magufuli alitoa maagizo hayo jana katika uzinduzi wa mfumo mpya wa
kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na
Kampuni ya Africom Tanzania.
"Tulianze
pale Kigamboni na tukaona mafanikio, tulipokuja hapa (Kigongo)
tukaboresha na mafanikio yameonekana kwa kiasi kikubwa. Vivuko vyote
sasa vifungwe mfumo mpya wa kielektroniki.vivuko vyote nchini,"
aliagiza Dkt. Magufuli.
Alisema
mfumo huo una faida kubwa ikiwemo kudhibiti upotevu wa mapato ambapo
katika kivuko cha kigongo - Busisi alisema mapato yameongezeka kwa
takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo.
Hata
hivyo, Dkt. Magufuli alikataa kutaja ni kwa shilingi ngapi mapato hayo
yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia wanaweza
kwenda na kufanya uhalifu.
Pia,
aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo wake kama
ilivyokuwa kwa Kigongo - Busisi. Waziri huyo wa Ujenzi, alisema kutokana
na mafanikio yanayopatikana katika kudhibiti upotevu wa mapato na
kurahisisha huduma kwa wananchi, wafanyakazi husika kwa maana ya wale wa
TEMESA maslahi yao yanapaswa kuangaliwa upya na kuboreshwa. "Kama
mapato ni mazuri, wafanyakazi nao walipwe vizuri, wasikae kimasikini
kwani wanapaswa kuona mwaka 2015 ni ukombozi katika maisha yao.
Alisema
serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete imefanikiwa kujenga
madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja 4880 nchini
na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo yalikuwa
ya kuvutwa.
Mfumo
wa kielektroniki katika vivuko vya Kigamboni na Kigongo Busisi
ulifungwa na Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji wake
Juma Rajabu alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti
upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao ndiyo
watumiaji.
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Na JIACHIE BLOG