Mabosi na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa katika tambiko hilo linalodaiwa kufanyika mapema wiki hii.
Za kitaa kutoka Mtwara zinadai kuwa bibi mmoja aliyeitisha Serikali kuwa ikifanya mchezo na haki za watu wa mkoa huo atabadili gesi kuwa maji, amewapigia tambiko Wafaransa wazungu wa Kampuni ya uchimbaji wa visima vya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd yenye ofisi zake Chole Road, Msasani Peninsular, Dar es Salaam, baada ya kile kilichodaiwa drill yao ya kuchimbia mafuta kukatika mara tatu wakati wakichimba kisima cha urefu wa mita 3,000 chini ya bahari. Inadaiwa baada ya kuanza kuona maajabu katika kazi yao hiyo, fasta walijisalimisha kwa bibi huyo huko Mtwara na kukubali kufanyiwa tambiko ili mambo yanyooke, kama wanavyoonekana pichani hapo juu! Kama ni kweli, basi bibi anatisha! Lol!!.