Japan inachunguza sauti
iliyorekodiwa ambayo inawezakana ni ya mwandishi wa habari wa Japan
aliyeshikiliwa mateka na wapiganaji wa Islamic state.
Sauti hiyo
inarudia tishio la kumuua rubani wa Jordan aliyetekwa mateka na
wapiganaji hao hadi Jordan itakapomwachia huru mwanamke wa Iran
aliyehusika shambulizi la bomu.Famili ya Rubani na mpiganaji mwenye asili ya Jordan anayeshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo wa hao wameendelea kuweka shinikizo kwa Serikali ya Jordan kufanya kila iwezalo kuokoa maisha yake.
Jordan imeahidi kumuachia mwanamke huyo lakiini Mjomba wa Rubani anasema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa wanamgambo wa IS kuwa hawataki kupokea ahadi hiyo na kuwa watamuua siku ya Alhamisi.
Baba na Mke wa Rubani huyo walikutana na mfalme wa Jordan, huku Familia na watu wa jamii yake walikusanyika nje ya kasri ya Mfalme, akizungumza nao katika eneo hilo nje ya Kasri ya Mfalme Abdullah, amewataka raia wa Jordan kuongeza shinikizo kwa Serikali ya Jordan kuhakikisha anachiuwa huru.
BBC