Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, wakiwa katika
Sala na Dua ya kumuombea aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa Bibi Fatma Othman Ali kabla ya mazishi yake iliyofanyika Januari
08,2015 katika msikiti wa Mohammed Ali Jang’ombe Zanzibar.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, wakisaidia
kutoa nje ya msikiti Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali baada ya Sala na Dua
maalum iliyofanyika Januari 08,2015 katika msikiti wa Mohammed Ali
Jang’ombe Zanzibar.Vijana
wa Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili
wa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman
Ali kuelekea katika makaburi ya Mwanakwerekwere Zanzibar kwa ajili ya
mazishi Januari 08,2015.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiweka Udongo kwenye Kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali wakati wa mazishi yake
yaliyofanyika Januari 08,2015 katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.
(Picha na OMR).