Makataa
yaliotolewa na mataifa ya maziwa makuu pamoja na jamii ya kimataifa kwa
wapganaji wa Hutu nchini Rwanda FDLR kusalimisha silaha zao
yanakamilika hii leo siku ya ijumaa.
Kufuatia kukamilika kwa ilani
hiyo,oparesheni ya kijeshi itakayotekelezwa na jeshi la DRC na
kusaidiwa na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa itaanzishwa
ili kuwapokonya silaha kwa nguvu.Kulingana na takwimu ni mmoja kati ya wapiganaji watano aliyesalimu kwa maafisa wa DRC,Kiwango ambacho kimedaiwa kuwa cha chini na mamlaka ya DRC,marekani pamoja na mataifa ya maziwa makuu.
BBC