Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Roberta Jacobson,ataongoza msafara wa wajumbe kutoka nchini mwake kuelekea Havana Cuba, baadaye mwezi huu,kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu ya kwanza kufanywa na nchi mbili hizo tangu kurejeshwa kwa uhusiano baina yao.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanywa mapema mwezi huu,na kutarajiwa kuangazia zaidi suala la uhamiaji.msafara huo unaongozwa na mwanadiplomasia Jackobson aliyebobea katika masuala ya Marekani Kusini ambaye pia anatarajiwa kuongeza msukumo katika mpango uliotangazwa na Rais Barack Obama pamoja na Raul Castrol juu ya uimarishwaji uhusiano.
Marekani ilisitisha uhusiano na serikali ya Cuba tangu mwaka 1961.