Wizara
ya sheria nchini Ubelgiji, imesema kuwa mwanamume aliyepatikana na
hatia ya mauaji na ubakaji sasa hatasaidiwa katika azma yake ya kutaka
kufariki kama alivyokuwa ameomba.
Katika taarifa ya wizara hio,
waziri Koen Geens, alisema, anaheshimu ushauri wa madaktari wanaomtibu
mtuhumiwa huyo aliyeiomba serikali kumsaidia katika kifo chake.Frank Van den Bleeken,aliwasilisha ombi lake kwa serikali kwambe asaidiwe kufa kwa kudungwa sindano yenye sumu ili kumwepushia msongo wa mawazo anaokabiliwa nao.
Kwa miaka mingi, mtuhumiwa huyo, alisema kuwa alishindwa kabisa kubadili au kukomesha tabia yake ya ubakaji na kutokana na hilo haoni uwezekano wowote wa kuachiliwa.
Uamuzi wa kesi hio, ni wa kwanza kumhusu mfungwa tangu sheria inayoruhusu watu wanaotaka kufariki kusaidiwa kufanya hivyo kuanza kutumika miaka 12 iliyopita.
BBC