Dominic
Ongwen, mmoja kati ya makamanda aliyekuwa na cheo kikubwa katika jeshi
la waasi wa Uganda Lord Resistance Army (LRA) ambaye pia alikuwa mtu wa
karibu sana na Joseph Kony, inataarifiwa amejisalimisha kwa kikosi cha
jeshi la Marekani kilichoko Africa ya kati ,na hii ni kwa muujibu wa
msemaji wa kikosi cha Marekani nchini humo.
Dominic alitekwa nyara
na LRA alipokuwa na umri wa miaka 10, na alikuwa akipanda vyeo katika
jeshi hilo la waasi na amekuwa akisakwa na mahakama ya uhalifu wa kivita
kwa makosa kadhaa yakiwemo ya mauaji ,uporaji,pamoja na utumikishaji.BBCSWAHILI