MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 26, 2015

NMB YADHAMINI MKUTANO MKUU WA MAKAMANDA WA POLISI KWA MILIONI 75.

 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Tom Boghols akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani – Mathias Chikawe hundi ya shilingi milioni 75 za udhamini wa Mkutano wa Mwaka Maofisa waandamizi wa polisi







   Waziri wa mambo ya ndani – Mathias Chikawe akimpongeza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu
   wa NMB – Tom Borgols kwa kujitoa kwa hali na mali kudhamini mkutano wa Maafisa wa Jeshi la
  Polisi unaoendelea mjini Dodoma mara baada ya kutoa ukumbini.




  Afisa kutoka NMB akimuelezea Mheshimiwa Waziri wa Ndani –Mathias Chikawe Juu ya     huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye banda la NMB.  

Benki ya NMB leo imekabidhi hundi ya shilingi Milioni 75 kama udhamini wa mkutano wa mwaka wa maafisa wa Polisi nchini unaendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa Kimataifa wa St Gasper.

Mkutano huo ambao unajumuisha makamishna, makamanda wa mikoa ya Tanzania bara na Visiwani pamoja na maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao makuu, umezinduliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Mathias Chikawe.

Akizungumza katika uzinduzi huo , Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Tom Borgols, alisema udhamini huo unajumuisha usafiri wa mabasi kwa washiriki wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani, pamoja na maandalizi ya mkutano huo.

“Jeshi la polisi ni wadau wetu muhimu ambao tumekuwa tukishirikiana nao kwa muda mrefu, sisi kama NMB tumefarijika sana kudhamini mkutano huu kwani kutoka katika mkutano huu, mipango na mikakati itakayojadiriwa itakuwa ni manufaa makubwa kwa nchi yetu pamoja na benki ya NMB ambayo matawi yake yote Zaidi ya 170 nchini kote yanapatiwa ulinzi kutoka jeshi la polisi.” Alisema Tom.

Katika maeneo ya ukumbi, NMB ina mabanda kadhaa ya maonyesho huku wakitoa huduma mbalimbali kama kutoa na kuweka fedha kupitia huduma ya NMB Wakala – huduma mpya inayoshirikisha mawakala wa MaxiMalipo, Kufungua akaunti kupitia Chap Chap Instant Account pamoja na elimu kwa ujumla juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.

Mkutano huo utadumu kwa muda wa siku 5 kuanzia leo Jumatatu tar 26 mpaka ijumaa tarehe 30 Mwezi huu.