Rais wa Marekani Barack Obama
amelaani kile alichokitaja kuwa mauaji ya kikatili ya mmoja wa raia wa
Japan aliyekuwa akishikiliwa mateka na wanamgambo wa Islamic State
Haruna Yukawa.
Rais Obama pia alitaka mateka mwingine anayeshikiliwa na wanamgambo hao mwandishi wa habari Kenji Goto kuachiliwa mara mojaKwa njia ya video Goto alionekana kwenye mitandao akishika mkononi picha ya maiti ya bwan Yukawa.
Mapema wataalamu mjini Tokyo na Marekani walisema kuwa wanatathmini ukweli wa picha hiyo.
Waziri mkuu nchini Japan Shinzo Abe alisema kuwa ameghadhabishwa na video hiyo.