MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 7, 2015

OFISI ZA MAGAZETI YA VIKATUNI PARIS ZASHAMBULIWA, 12 WAUAWA

Maofisa wa polisi jijini Paris, Ufaransa wakiwa nje ya ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Vikatuni ya Charlie Hebdo baada ya shambulizi.

Ofisi za Charlie Hebdo zilizoshambuliwa leo.
Katuni iliyowekwa kwenye akaunti ya Twitter ya Charlie Hebdo ikimuonyesha Kiongozi wa Kundi la Wapiganaji wa Islamic State, Abu Bakr al-Baghdadi.
Baadhi ya majeruhi katika shambulio hilo wakipatiwa huduma ya kwanza.
Tundu la risasi katika ofisi hizo.
WATU 12 wameuawa, saba wakijeruhiwa baada ya ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Vikatuni ya Charlie Hebdo zilizopo jijini Paris, Ufaransa kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kali leo.
Mashuhuda wa tukio hilo wanadai watu wawili waliokuwa na bunduki aina ya AK 47 wakiwa wamevaa 'mask' waliingia katika ofisi hizo na baada ya muda mfupi walisikia milio ya risasi.
Shuhuda huyo aliongeza kuwa mashambuliaji hao walikuwa wakiongea kwa sauti maneno haya:"Tumelipiza kisasi kwa aliyotendewa Mtume Muhammad"
Wakati washambuliaji hao wakitokomea kwa gari walipambana na polisi mitaani japo hawakukamatwa.
Shambulio hilo linadaiwa kuwa ni kulipiza kisasi kwa Kundi la ISIS baada ya hivi karibuni kampuni hiyo ya magazeti kuweka katuni ya Kiongozi wa Kundi la Wapiganaji wa Islamic State, Abu Bakr al-Baghdadi kwenye akaunti yao ya Twitter.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amesema shambulio hilo ni la kigaidi.
Polisi jijini Paris wamezagaa mitaani kuhakikisha wanawakamata wauaji hao.