“Hongera sana mdogo wangu kwa ushindi mwaka 2014 #chausiku Nakuombea
Kila la kheri katika mwaka huu wa 2015 uzidi kufanya vizuri zaidi
inshallah amin Nakupenda sanaaaaaaaaaa na kukabidhi rasmi mikoba mamie".
Riyama aliyaema hayo baada ya kubandika picha hiyo wakiwa ndani ya
studio za redio Clouds FM mara baada ya filamu ya Chausiku iliyochezwa
na mwanadada Shamsa Ford iliyotoka miezi ya mwishoni mwa mwaka jana,
kutangazwa ndio iliyoshika namba moja huku filamu ya Kigodoro ikishika
namba mbili.