MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 8, 2015

Sanaa ya sarakasi yainua vijana TZ

Nchini Tanzania si jambo la ajabu kuona Watoto na wakubwa wakicheza sarakasi mitaani.lakini sifa hii ya kuwa nchi maarufu kwa sarakasi barani Afrika inatoka wapi, Mwandishi wa BBC alizuru Dar es Salaam kubaini hayo.
Mcheza sarakasi Raia wa Zimbabwe Winston Ruddel alianza kusaka vipaji kwa ajili ya taasisi yake iitwayo Mama Afrika, kituo chake cha kwanza kilikua jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania, huko alianzisha shule ya Sarakasi, Mama Afrika
''Awali ilikua kama nilifanya makosa'', anaeleza Ruddel.'' nilipewa Mkataba mjini Las Vegas kwa ajili ya maonyesho ya sarakasi, hivyo nikaja Tanzania kutafuta vijana walio na ufahamu na mchezo wa sarakasi, tukafanya kazi pamoja, lakini wamarekani hawakuvutiwa na vijana wale. Tayari nilishawaahidi mkataba, hivyo nikaanza kuwatafutia kazi.,wishowe,tulipata kazi nyingi zilizonilazimu kufungua shule ili kukidhi mahitaji.ilianza kwa kosa dogo lililozaa mafanikio makubwa''.

Mmoja kati ya waliofundisha katika shule hiyo, Selemani Mohamedi Nomondo, anasema ''nilianza kunyonganyonga viungo vyangu nikiwa na umri wa miaka mitatu, ikiwa utaanza mapema zaidi, mwili wako utazoea na hutasikia maumivu, kwa kutazama inaonekana ngumu, kuliko uhalisia ulivyo''.
Maonyesho ya Mama Afrika hutumia muziki katika kazi zake jukwaani, pia shuleni wakati wa mafunzo. Ngoma ni kiini cha mchezo wa sarakasi huwapa wasanii ari ya mchezo na kusaidia katika uchezaji kwa wanakikundi.
Rajab Zubwa anasema yeye ni mtu wa kwanza kuwa mwanasarakasi '' nilisoma kwa miaka minne nchini China miaka ya 1960.Tanzania na China walikuwa na uhusiano wa karibu wa kisiasa hivyo Serikali zote mbili zilianzisha mafunzo ya kubadilishana, anaeleza'' nilipata faida kubwa nilipokuwa kwenye shule ya Sarakasi na niliporejea nilikuwa mwalimu wa sarakasi.
Maonyesho ya Mama Afrika mpaka sasa yamefanyika katika mabara matano, ikiwemo mjini New York.kuna maonyesho mengi yanafanyika kwa wakati mmoja , lakini sio rahisi kuwa sehemu ya maonyesho ni wahitimu wanye uwezo wa juu pekee kutoka kwenye shule hiyo hufanikiwa kufika katika hatua ya kimataifa.
Watoto wanakaribishwa katika shule ya Mama Afrika wakati wa mwisho wa wiki na wanapokua likizo.
Tangu shule hii ilipoanzishwa mwaka 2003 zaidi ya wanafunzi 300 walimaliza masomo yao.wengi walianza kufanya maonyesho mbali mbali ya sarakasi, wengine walijiunga na Kampuni za sarakasi duniani.
Pamoja na tamaduni za micheo hii nchini Tanzania, programu za shule hazidhaminiwi na Serikali wala Sekta binafsi, shule ya Ruddel iko maeneo ya Magomeni moja ya eneo waishio watu wengi wa kipato cha chini jijini Dar es Salaam, baada ya kazi ngumu ya mafunzo wanafunzi hupata chakula.
''Jina langu Tumaini, mimi ni Mshonaji nguo wa Mama Afrika.huwa tunavaa nguo halisi za kiafrika jukwaani, tunatumia vitambaa vizuri ambavyo huvaliwa mitaani.
Naitwa Deborah Dixon ni mmoja kati ya wasichana wachache ambao hufanya sarakasi kwa mtindo wa kukunjakunja viungo.wasichana wengi hupenda kufanya sarakasi kwa mchezo wa kucheza ngoma kwa sababu ya tamaduni za kifamilia si sawa kwa watoto wao wa kike kutanua miguu na kugalagala kwenye sakafu.kwa upande wangu kukunjakunja viungo ni sanaa .
Ally Kibwana Ally anasema'' kwangu mimi kuwa na Mama Afrika kunamaanisha kuwa niliweza kuishi kutegemea kipaji changu. Nimetembelea sehemu nyingi duniani na kujifunza mengi.sasa ninatoa ujuzi huo kwa Wanafunzi wengine ili nao waweze kupata nafasi kama mimi''.
Anaongeza; ''tofauti kubwa kati ya wasanii hapa na maeneo mengine duniani ni kuwa hapa Watu wanafurahia wanachokifanya.Inawezekana tukawa hatuna ujuzi na utaalam kama ilivyo kwa wasanii ya China na Urusi lakini tunanguvu inayotuunganisha na hadhira.''