Serikali ya Urusi inasema kwamba Rais wa Korea Kaskazini amekubali mwaliko wa Rais wa nchi hio kuzuru Urusi.
Taarifa hii ni ka mujibu wa shirika la habari la Yonhap nchini humo.Shirika hilo la habari limenukuu ujumbe kutoka kwa ikulu ya Urusi, Kremlin ingawa taarifa hio haijamtaja rasmi Kim Jong-un.
Hata hivyo Yonhap linamnukuu afisa mmoja wa wizara akisema kumtaja kiongozi huyo haina umuhimu wowote.
Kim Jong-un hajafanya ziara katika nchi za kigeni tangu kuchukua mamlaka mwaka 2011.
Kituo chake cha kwanza kitaangaliwa kwa karibu sana kwa sababu ya kile wnegi wanasema ni sera zake kanadmizi.
Mapema mwezi huu, taarifa zilisema kwamba Urusi ndio itakuwa nchi ya kwanza kumwalika Rais Kim.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov aliambia wandishi wa habari kuwa mnamo tarehe 21 mwezi Januari, Rais Kim atapewa mwaliko wa kwenda Urusi kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa vita vya pili vya dunia zitakazofanyika tarehe 9 mwezi Mei.
Alisema kuwa dalili ya kwanza kutoka kwa serikali ya Korea Kaskazini inaonyesha mambo yako shwari.
Shirika la habari la Yonhap lilisema kuwa majibu wa taarifa kutoka kwa ofisi ya Rais wa Urusi, Rais wa Korea Kaskazini ni mmoja wa viongozi walioalikwa kutoka nchi 20 na ambao wamethibitisha kuhudhuria sherehe hizo.
Lakini barua hiyo haikuthibitisha ikiwa Rais Kim ni mmoja wa walioalikwa wala ikiwa amekubali mwalikoi huo kwani ilisema: ''Orodha ya watakaohudhuria haijakamilishwa, tunaendelea na mikakati ya kuthibitisha wakaohudhuria
Hapajakuwa na taarifa rasmi kutoka kwa serikali ya Korea Kaskazini kuhusu tetesi hizo.
Kim Yong-nam, ambaye kikatiba ni Rais asiye na mamlaka wa nchi hio ndiye amekuwa akiwakilisha Korea Kaskazini katika mikutano katika nchi za kigeni.
Ziara za marehemu babake Rais Kim, Kim Jong-il, hazikuwa zikitangazwa hadharani kabla ya yeye kuondoka nchini humo.