Utafiti mpya unasema aina nyingi za
ugonjwa wa saratani ni matokeo ya bahati mbaya, kuliko malezo ya
vinasaba, mazingira na mtindo wa maisha.
Watafiti nchini Marekani
walichunguza aina 31 za saratani na kugundua kwamba theluthi mbili
zilisababishwa na mgawanyiko holela wa seli. Kwa mgawanyiko wa kila seli
kuna hatari ya mabadiliko yanayoweza kusababisha saratani.Wanasayansi hao wanasema kuimarisha mtindo wa maisha na mazingira kunasaidia kudhibiti magonjwa kama ya saratani ya ngozi na saratani ya mapafu.
BBC