MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 30, 2015

Viongozi wa Afrika wakutana Ethiopia

Mkutano wa wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika unaanza leo nchini Ethiopia ambapo viongozi wa Afrika wanatarajiwa kujadili masuala muhimu yanayolikumba bara la Afrika kwa sasa.
Baadhi ya maswala yatakayopewa kipaombele kwenye mkutano huo niharakati za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, pamoja na juhudi za kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Licha ya kauli mbiu ya mkutano huo wa siku mbili kuwa swala la kuwawezesha wanawake, viongozi kutoka nchi 54 wanachama wa Muungano huo watalazimika kangazia swala la migogoro ambalo limekluwa changamoto kubwa kwa bara la Afrika.
Mwenyekiti wa muungano huo, Nkosazana Dlamini-Zuma amepigia debe swala la umoja katika kupambana na wapiganaji wa kiisilamu wanaoendelea kuteteresha amani katika bara hilo.
Mnamo siku ya Alhamisi, baraza la usalama na amani la AU, lilitoa wito wa haja ya kuwepo kikosi cha wanjeshi 7,500 kupelekwa katika maeneo yanayokumbwa na migogoro Afrika.
Wakati huo huo Kenya inatarajia kutuma ujumbe mzito kwenye mkutano huo kama mwanzo wa hatua yake ya kukata uhusiano na Mahakama ya jinai ICC.
Katika kikao kilichopita cha Umoja wa Afrika kilichokaa mjini Malabo Equatorial Guinea wajumbe walisaini mkataba wa uundwaji wa mahakama ya Afrika itakayoshughulikia kesi za Afrika badala ya kuzipeleka kwenye mahakama ya ICC, baadhi yao wakidai kuwa kesi za mahakama hiyo zinawalenga waafrika pekee.

BBC