Ripoti kutoka Mali zinasema kuwa walinda amani wa umoja wa mataifa katika mji wa kazkazini wa Gao wamewafyatulia risasi waandamanaji na kuwaua watu watatu.
Maelfu ya waandamanaji walikongamana nje ya kambi ya vikosi vya umoja wa mataifa huku baadhi yao wakirusha mawe.
Walikasirishwa na ripoti za kutaka kubuni eneo ambalo litawatenga wapiganaji wa pande pinzani katika eneo hilo ambalo wanaamini litapendelea waasi wanaotaka kujitenga wa Tuareg.
Hakujatolewa tamko lolote na umoja wa mataifa nchini Mali.
Kikosi hicho chenye wanajeshi elfu kumi kilibuniwa takriban miaka miwili iliopita baada ya vikosi vya Ufaransa kuwazuia waasi wa kiislamu kutoufikia mji mkuu wa Bamako.