Washukiwa wa mauaji ya wachora vibonzo nchini Ufaransa, wanadaiwa kufanya wizi katika kituo cha mafuta Kaskazini mwa Ufaransa huku wakiwa mbioni kutorotoka polisi.
Inaarifiwa washukiwa hao wawili ambao ni mandugu, waliiba chakula na petroli huku wakifyatua risasi karibu na eneo la Villers-Cotterets.
Watu nchini ufaransa wamesimama kimya kwa dakika moja kwa heshima ya watu 12 waliouawa na watu wenye silaha walipovamia gazeti moja la vichekesho la Charlie Hebdo siku ya Jumatano
Huku polisi nchini ufaransa wakiendelea kuwatafuta wanaume walioshambulia gazeti la vichekesho la Charlie Hebdo siku ya Jumatano kumeripotiwa kutokea shambulizi lengini mjini Paris
Afisa wa kike wa polisi aliuawa wakati mwanamume mmoja alipomfyatulia risasi eneo moja kulikotokea ajali ya barabarani.
Kwa sasa polisi wanawatafuta wanaume watatu lakini bado haijabainika ikiwa kuna uhusiano kati ya tukio hilo la pili na la awali kwenye gazeti la Charlie Hebdo ambapo polisi wanaamini liliendeshwa na ndugu wawili.
Watu wengine saba wanaokisiwa kuwa na uhusiano na washukiwa hao bado wanazuiliwa na polisi.
Waziri mkuu nchini Ufaransa Manuel Valls anasema kuwa washukiwa hao (Said Kouachi na Cherif Kouachi) walikuwa wakifahamika kwa mashirika ya kijasusi.
Akiongea baada ya mkutano na rais wa ufaransa, mkuu wa chama cha upinzani cha UMP na raisi wa zamani Nicolas Sarkozy amesema kuwa shambulizi hilo ni la kinyama.