Takriban Watu 12 wameuawa na watano kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na watu wasiojulikana.Shambulio hilo lililitekelezwa kwenye ofisi ya gazeti la Charlie Hebdo jijini Paris nchini Ufaransa.
Watu wenye silaha waliingia kwenye jengo na kuanza kufyatua risasi wakiwa na silaha ambapo inaelezwa milio takriban hamsini ya risasi ilisikika, kisha Watu hao walikimbia kwa gari.
Polisi wanafanya jitihada za kuwapata waliohusika na shambulio hilo. Mji wa Paris umewekwa katika taadhari kubwa ya kiusalama.