MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 6, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya  umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw.  Steve Thomson (kushoto)
 Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na  wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani)
 Mkazi wa kata ya Ijitu  iliyopo wilayani Busega ambaye  jina lake  halikupatikana mara moja akitoa hoja yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto  waliosimama mbele) mara Waziri alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi
Diwani wa Kata  ya  Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti  akielezea kero za umeme katika kata yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto), viongozi na wananchi  (hawapo pichani).
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka  Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika  Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara  katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi  ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu  cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza  ziara  katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini  pamoja na kuzungumza na wananchi.
 Mkazi wa kijiji cha  Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu   ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali  mbele ya  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi  (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya  mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo  kwenye mkutano  na  wananchi wa  kata ya  Ijitu iliyopo wilayani Busega
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma ( wa mwisho kushoto)  ya kuitaka  Tanesco kuongeza kasi ya  usambazaji wa umeme  vijijini.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo   katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha  Bushigwamala  wilayani Busega (hawapo pichani)
 Sehemu ya umati wa wananchi wa kata ya Kalemala wilayani Busega waliojitokeza kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakifuatilia kwa makini hotuba yake.