Nyaraka zilizofichuliwa kwa BBC na
vyombo vingine vya habari zinaonyesha kuwa moja ya benki kubwa zaidi
duniani HSBC, imekuwa ikiwasaidia wateja kukwepa kulipa kodi.
Maelezeo
kutoka kwa maelfu ya akaunti katika benki hiyo ya HSBC nchini Uswizi,
yanaonyesha kuwa wafanyikazi waliwashauri wateja wake wakiwemo
wanasiasa, Wahalifu na watu mashuhuri jinsi ya kuhifadhi fedha bila
kulipa kodi katika akaunti hizo kutoka kwa zaidi ya mataifa 200.Akaunti kama hizo zimekuwepo tangu mwaka 2007 na benki hiyo inasema kuwa wengi walitumia usiri wake kuwa na akaunti zisizotambuliwa.
Kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband, anasema kuwa serikali ya Uingereza ina maswali chungu nzima ya kujibu
BBC