Katibu Mkuu wa NATO, Jens
Stoltenberg amesema kuwa Urusi inaendelea kukiuka Sheria za kimataifa
wakati huu mapigano yakiendelea nchini Ukraine.
Kauli hiyo
imetolewa wakati Mawaziri wa Ulinzi kutoka jumuia ya NATO walipokutana
mjini Brussels kujadili namna ya kuliimarisha Jeshi hilo, hatua ambayo
inaelezwa kuwa kubwa tangu baada ya Vita baridi.Wakati huohuo,Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani,John Kerry anatarajiwa kufanya mazungumzo mjini Kiev wakati ambapo Marekani inafikiria uwezekano wa kupeleka Silaha kuisaidia Ukraine kupambana na Waasi wanaounga mkono Urusi.
Kikosi cha Wanajeshi 5000 kinatarajiwa kutangazwa, na maeneo watakayokuwa,Stoltenberg amesema mabadiliko haya yanatokana na Mazingira ya kiusalama yalivyo kutokana na kile alichokiita ushari wa Urusi.
Nato pia itaweka wazi mipango yake ya kuanzisha Matawi nchini Estonia,Lithuania,Latvia,Poland,Romania na Bulgaria.