Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani
ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro miwshoni mwa juma.
Balozi
wa Jumuiya ya Ulaya nchini, Filiberto Ceriani Sebregondi akisoma risala
wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo
kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiteta jambo Rais Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete mara baada ya zoezi la picha ya pamoja wakati wa sherehe
za kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akisalimiana kwa furaha na Mkuu wa wilaya ya Morogoro mjini, Jordan
Rugimbana wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya
wanawake duniani ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Morogoro.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akifurahi jambo
wakati akiwapongeza Sister Stella Mgaya (wa pili kulia) wa Kituo cha
kupambana na ukeketaji cha Masanga (TFGM) Tarime, mkoani Mara na
Mkurugenzi wa Kituo hicho, Sista Germaine Baibika (wa pili kushoto)
baada ya kutunikiwa tuzo ya kutambua mchango wao wa kupambana na
ukeketaji kwa wasichana wilayani Tarime. Kulia ni Balozi wa Jumuiya ya
Ulaya nchini, Filiberto Ceriani Sebregondi.
Msanii
nguli wa muziki nchini, Starah Thomas akiimba wimbo maalum katika siku
ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo kitaifa ilifanyika mkoani
Morogoro.
Msanii
Peter Msechu akitoa burudani sambamba na baadhi ya wanafunzi wa shule
za sekondari Morogoro kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa
ya wanawake duniani ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.
Wanafunzi
mbalimbali wa shule za sekondari mkoani Morogoro wakifurahia burudani
zilizokuwa zikitolewa kwenye uwanja wa Jamuhuri yalipofanyika
maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kufikia kilele chake machi 8
mwaka huu.
Kudhihirisha
kuwa hata wanawake wanaweza: Mtaalamu wa Danadana Tanzania nzima
hakuna, Hazala Charles Mnjeja a.k.a Ronaldo akitoa burudani kwenye
kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa Morogoro waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya
siku ya wanawake duniani wakiwemo kina baba ambapo kitaifa ilifanyika
mkoani Morogoro.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (kushoto) na Afisa Habari wa Ubalozi wa Jumuiya ya Umoja wa ulaya
Tanzania (EU), Susanne Mbise wakiwa kwenye picha ya pamoja na mtoto
Miriam Edward aliyeambata na mama yake mzazi ndani ya viwanja vya
Jamuhuri kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Morogoro.
Baadhi
ya raia wa kigeni na wakazi wa Morogoro wakiingia kwenye lango kuu la
uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro kushiriki sherehe za siku ya wanawake
duniani.
Rais
wa VICOBA, Tanzania Bi. Devotha Likokola akizungumza na baadhi ya
vikundi mbalimbali vya wanawake vilivyoshiriki kwenye maonyesho ya siku
ya wanawake duniani mkoani Morogoro na kuwataka kujiunga na VICOBA ili
waweze kupanua mitaji na wigo wa biashara zao.
Afisa
Utumishi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Mashariki
Esuvatie Masinga akitoa elimu ya kutambua Haki na wajibu kwa mdau wa
mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwenye banda lao wakati wa maadhimishi
ya siku ya wanawake duniani ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.
Afisa
Habari wa Jumuia ya Umoja wa ulaya Tanzania (EU), Susanne Mbise
akijadiliana jambo na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) pamoja na Stephaine Raison
ambaye ni Afisa Mawasiliano wa UN Women (Katikati).
Mgeni
rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete kwenye picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha
nchi zao Tanzania pamoja na viongozi wa serikali.