Faiza Ally katikati akiwa ameshika sink la choo tayari kwa msaaa wa shule
“Tumefurahi tumefanikiwa tulijichangisha tukaweza kununua vyoo 10 kwa ajili ya kusaidia watoto wa shule ya mwananyamala kisiwani- ninajisikia very proud na team yangu”-
Faiza aliandika mtandaoni mara baada ya kubandika picha hizo hapo juu wakiwa shuleni hapo.
“Watoto wamefurahi final wataingia kwenye vyoo visafi na salama”-Faiza aliandika akiwa pamoja na watoto hao.
Pia Faiza aliwashukuru watu wengi ambao walimpongeza na kumpa moyo na kuahidi kuwa ataendelea kufanya hivyo.
“Asanteni wote kwa pongezi zenu - comment zenu ni zuri kwetu maana zinatupa moyo wa kufanya tena na tena Insha Allah”
Bongomovies.com pia inakupongeza kwa moyo wako wakusaidia jamii, ni mfano mzuri umeuonyesha ukiwa kama kioo cha jamii, Mungu akuongezee pale palipopungua.