Staa wa Bongo Movies ambae ni mwigizaji na mwogozaji wa filamu,Jacob
Stephen ‘JB’ amesema ukosefu wa wandishi wazuri wa script kuwa ni moja
kati ya matatizo yanayoikambili tasnia ya filamu hapa Bongo, akitolea
mfano wa wewe kutafuta script kwa muda sasa bila mafanikio.
“Moja ya matatizo makubwa tuliyonayo kwenye tasnia ya filam ni
waandishi wa script, hatuna waandishi wa kutosha, jamani mbona wasomi wa
fani hii wapo, nina miezi mitano natafuta script sijapata, ukiletewa ni
vituko nazungumzia script sio story maana hizo ziko nyingi na
ukinipigia simu hakikisha wewe ni mwandishi mwenye taaluma hiyo
nikiipenda script yako nitanunua kwa bei yoyote “. JB ameeleza.
Haya fursa ndio hiyo kwa wenye uwezo.
KWA HISANI YA BONGO MOVIES.COM