MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Mar 9, 2015

MWANA HIP HOP FLABBA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MPENZI WAKE AFRIKA KUSINI

Nkululeko Habedi maarufu kwa jina la Flabba enzi za uhai wake.
Flabba (wa kwanza kushoto waliochuchumaa) akiwa na wanamuziki wenzake wa Skwatta Kamp.
MWANA Hip hop wa Afrika Kusini, Nkululeko Habedi maarufu kwa jina la Flabba (38) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtu anayedaiwa kuwa mpenzi wake akiwa nyumbani kwake Alexandra jijini Johannesburg.

Flabba ameuawa mapema leo na mwanamke huyo tayari yupo mikononi mwa polisi.
Polisi nchini humo wameeleza kuwa mpenzi wa Flabba atashitakiwa kwa mauaji na atapandishwa kizimbani ndani ya saa 48.
Rappa huyo alipata umaarufu baada ya kujiunga na Kundi la Skwatta lililoanzishwa miaka ya 1990.
Wanafamilia, marafiki na mashabiki wametoa salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii hasa Twitter.
Juu ni taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini kuhusu kifo cha rappa huyo.