Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akisalimiana na meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Mesharck Bandawe pindi alipowasili jana Kahma mkoani Shinyanga kutoa pole kwa waathirika wa mvua zilizoambatana na upepo eneo la Mwakata wilayani humo. |
Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe (kulia) akikabidhi msaada wa simenti na mabati kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya kwaajili ya wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. |
Jumla ya mabati 112 yamekabidhiwa kama sehemu ya msaada. |
Nayo mifuko 100 ya simenti ni sehemu ya msaada toka PPF. |
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya (kushoto) akitoa shukurani kwa PPF kupitia Meneja wake Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe (kulia) mara baada ya kukabidhiwa msaada wa simenti na mabati kwaajili ya wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. |
PPF. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa na wilaya kutembelea maeneo ya kata za wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. |
Ukuta umeanguka paa liko mashakani. |
Hali tete. |
Salaaam .....poleni. |
RAIS Jakaya Kikwete amesema
Serikali itajenga nyumba 403 ambazo zimebomolewa na mvua kubwa
iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na
kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi.
Kauli
hiyo aliitoa jana kwenye kijiji cha Mwakata baada ya kutembelea eneo
lililoathiriwa na mvua hiyo na kujionea maisha duni wanayoishi watu hao.
Akizungumza
na wananchi waliohudhuria mkutano wake Rais Kikwete alisema Serikali
iko pamoja na wananchi hao na itahakikisha makazi yao yanarejea katika
hali yake ya kawaida kwa kuwajengea nyumba hizo.
Pia, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wajenge
nyumba hizo bila kupitia mkandarasi yeyote kama vile ulivyo ujenzi wa
Serikali kwa kuwa ujenzi wa jeshi unaisha kwa muda mfupi na hakuna
uchakachuaji.
Aliwataka
viongozi mkoani Shinyanga kuhakikisha ujenzi huo hautangazwi na kuagiza
JKT kwenda kwenye eneo hilo kufanya tathmini ya ujenzi huo ili uanze
mara moja.
Rais
Kikwete aliwatoa wasiwasi wananchi wa Mwakata waliokumbwa na tatizo
hilo kwamba Serikali itahakikisha wote wamepata chakula hadi mwisho
watakapolima na kupata mavuno na tukio hilo wasilihusishe na imani za
kishirikina.
Alisema
mvua hizo ni za kawaida ambazo hutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi
na si ushirikina hivyo aliwataka wananchi hao waendelee kuwa na hisia
hizo lakini wasilichukulie kwa uzito swala la ushirikina wakatafuta
mchawi wa mvua hiyo
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga alimwambia
Rais Kikwete kwamba mvua hiyo licha ya kuua watu 47 pia imeharibu mazao
hekari 2,332 pamoja na visima 53 vya maji ya kunywa.
Rufunga
alisema mpaka kufikia sasa wahisani mbalimbali wamechangia kwenye tukio
hilo Sh64 milioni pamoja na tani 63 za unga wa sembe pamoja na mahitaji
mbalimbali ya kibinadamu yakiwamo mabati zaidi ya 1,000
HABARI KWA HISANI YA GSENGO BLOG