Mrembo na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu ametoboa kuwa wimbo wa
“Ntampata Wapi” ulioimbwa na aliekuwa mpezi wake, Diamond Platnumz
hakuimbiwa yeye, hii ni kutokana na watu wengi kudhani kuwa wimbo huu
alitungiwa yeye ukizingatia kuwa wakati wimbo huo unatoka ndio kilikuwa
kipindi wametoka kuachana.
“Leo nasema rasmi kuwa hii nyimbo hakuniandikia mimi….because
nilikuwa naisikia hii nyimbo hata wakati tulipokuwa kwenye uhusiano
amekuwa akiimba, akiindika kwahiyo ilikuwa tu ni moja ya nyimbo zake
kama anavyoandika nyimbo zote lakini nadhani tu timing ya kutoka ndio
kidogo imekuwa na utata because kaitoa timing ambayo watu wote wakadhani
kamuimbia Wema but in real sense noo,” aliongeza Wema.
Wema ameyasema hayo hivi majuzi alipokuwa jijini Arusha wakati
akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Radio 5 cha jijini humo.