Sehemu
ya umati wa Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kumsikiliza
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani),wakati alipokuwa
akiwahutubia wananchi hao na kuwaasa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha
ili kupata nafasi ya kushiriki katika upigaji kura ya maoni ya Katiba
inayopendekezwa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kata
ya Itolwa mara baada ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo na kushiriki katika shughuli za ujenzi wa maendeleo wilayani
Chemba ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi
CCM, Pamoja na kuhimiza uhai wa chama hicho.
Katibu
Mkuu Kinana katika ziara hiyo anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi CCM na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa wa
Dodoma, Kinana ataendelea na ziara kesho katika wilaya ya Kondoa Kabla ya kuendelea katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Mbunge
wa Jimbo la Chemba (kondoa kusini),na Naibu Waziri wa
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh Juma Nkamia akizungumza na
wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Itolwa Wilayani
Chemba,Mh.Nkamia kupitia Wizara yake alikabidhi hundi za fedha zenye
thamani ya shilingi Milioni 52 kwa vikundi tisa vya vijana
vinavyojishughulisha na ujasiliamali.Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Kinana (pichani shoto) pia aliwahutubia wananchi hao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika uwanja wa Itolwa wilayani Chemba mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mrijo wilayanii
Chemba,alipokwenda kukagua mradi wa ujenzi wa soko la Kimataifa,Wiayani
Chemba mkoani Dodoma.
Wananchi
wa Kijiji cha Babayu wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Chemba tayari kuendelea na ziara
yake ya siku tisa mkoani Dodoma
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) akishiriki kazi ya
kupiga misumari katika paa la jengo la ofisi ya serikali ya kijiji cha
Babayu,Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mh. Chiku Galawa kushoto na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Dodoma Mh. Adam Kimbisa wakipiga plasta katika ukuta wa josho
linalokarabatiwa katika kijiji cha Gwandi.Mradi huo mpaka kukamilika
utatumia zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 11.Josho hilo lilijengwa mwaka 1969 na Mwalimu J.K Nyerere
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa
amekaa chini kwenye kigoda wakati akipakwa na kuvishwa mgorole ikiwa
ni kama ishara ya amani upendo,baraka na heshima ya wazee wa Chemba.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pichani shoto akitoka kupanda mti na kukagua
wodi ya akina Mama na Watoto,itakayokuwa ina uwezo wa kuwahudumia
wanakijiji wapatao zaidi ya elfu moja kilichojengwa katika zahanati ya
Kelema,wilaya ya Chemba,Mradi wa ujenzi wa jengo hilo ni ulianza mnamo
mwaka 2013 na kutarajiwa kumalizika mnamo mwaka 2015,ambapo zitatumika
kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 42
Baadhi ya ya wafuasi wa CCM wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Mapango
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Mapango,wilaya ya Chemba,ambapo walieleza tatizo lao kubwa
linalowakabiri katika kijiji hicho ni ukosefu wa maji,ambapo katibu
Mkuu,Kinana aliahidi kuhakikisha kijiji hicho kinapata maji safi na
salama kwani tayari utandikaji wa mambomba ya maji ulikwishaanza.
Mmoja wa wananchi akiwa amebeba picha ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijji cha Songolo,walipokuwa wakimpokea.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wananchi
katika kijiji cha Songolo,walipokuwa wakimpokea.
katika kijiji cha Songolo,walipokuwa wakimpokea.
Katibu
Mkuu wa CCM,akiondoka kwenye mkutano mara baada ya kuwasalimia wananchi
katika kijiji cha Songolo,kulia kwake ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Dodoma Mh.Adam Kimbisa