Serikali ya Ufaransa imesema kuwa
inangojea jibu kutoka kwa kanisa Katoliki kuhusu uajiri wa balozi wa
mapenzi ya jinsia moja katika makao makuu ya kanisa hilo mjini Vatican.
Msemaji wa serikali hiyo amesema kuwa Ufaransa haitaondoa uteuzi wake wa Laurent Stefanini ambao ulifanywa mwezi Januari.Waangalizi wanasema kuwa uteuzi wowote unaofanywa na kanisa katoliki huthibitishwa kati ya mda wa wiki sita na kwamba kimya hicho kikuu kinaamaanisha kwamba uteuzi huo umekataliwa.
Uteuzi huo unaonekana kama mtihani kwa upande wa Papa francis ambaye amekuwa na msimamo ulio huru kuhusiana na wapenzi wa jinsia moja.
bbc