MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

May 30, 2015

HOJA DHAIFU NA ZA KITOTO SANA ASEMA Jonas Shija Ilamla BAADA YA HOTUBA YA MHE: LOWASSA



Jonas Shija Ilamla
Nasikitika sana kwa mkutano ulioandaliwa kwa mabilioni ya shilingi halafu hakuna jipya wala geni hata maana wa yote aliyoyaongea Lowassa. udhaifu wa hotuba hii ni kama ifuatavyo:
1. Hajasema mkakati hata mmoja wa kila jambo analoona halijaenda vizuri mfano amesema ataondoa UMASKINI bila kusema hata kwa kugusia tu ataondoaje umaskini. Kipimo hiki sioni kama huyu mtu anao upeo wa kutosha kushughulikia umaskini wa watanzania

2. Amesesma atapiga vita rushwa kwa vitendo, Ni kichekesho sana kwa mtu mwenye kashfa za Richmond, ICC, Jeshini na Jengo la UVCCM ambayo anapaswa kuyatolea ufafanuzi halafu anasema atapiga vita rushwa. Ndugu watanzania tujiulize akina KARAMAGI na kashfa zao za TICTS na RICHMOND hao ndo wadhamini wake sasa rushwa itakwisha au itaongezeka? Jambo moja amesema kuwa ANAGOMBEA URAISI ILI KUUMALIZA UMASKINI m\kwake na kwa familia na marafiki zake kwani wataiba mpaka wawe mabilionea
3. Kukejeli viongozi wake wa juu hasa Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mhe. Mangulla eti watu wakishangilia atapata hoja ya kumshughulikia na ametamka mara nyingi sana.
4. Suala la KUBEZA KILIMO ameliendeleza. Nadhani hana uelewa wa kutosha juu wa suala la kiuchumi. Uingeleza anayoitolea mfano leo walifanya MAPINDUZI YA VIWANDA KARNE YA 18 ndo maana leo ELIMU kwao ni kipaumbele namba moja hadi Tatu, lakn LOWASSA amesahau kuwa zaidi ya 78% ya watanzania wanategemea KILIMO na ili uondoe umaskini ni lazima ushughulike na sekta yenye watu wengi wala sio kuchukua mawazo ya ulaya uyalete huku kwetu wakati huko hawaongelei habari ya njaa, habari ya barabara n.k
4. Maamuzi magumu maamuzi magumu kwa lipi hasa? Ni maamuzi magumu yapi hasa LOWASSA kafanya? Maamuzi magumu sio sera ya kupata maendeleo ya nchi yetu. tunataka RAIS atakae jibu maswali watanzania waliyonayo na atuambie atayakabilije? Sio kwa kuongea maneno bila MIKAKATI jaman


CHANZO NA Jonas Shija Ilamla FACEBOOK

0757 487 262