MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

May 2, 2015

LUKU YAZUA GUMZO NCHINI

Pichani ni baadhi ya wakazi wa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar, wakiwa kwenye foleni ya kununua umeme wa luku kwenye kituo cha Sayansi, Kijitonyama baada ya kupatwa na kwikwi kwa siku kadhaa zilizopita kwenye vituo vingine pamoja na kwenye mitandao ya simu.ila sasa Tanesco wametoa taarifa na kusema mambo yako mswano kwa sasa.

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) 
 TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA LUKU KWA BAADHI YA MAWAKALA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatoa ufafanuzi juu ya tatizo lililojitokeza kwa baadhi ya mawakala wa LUKU kushindwa kutoa huduma ya kuuza umeme. Hali hiyo inatokana na Kampuni ya Selcom ambaye ni wakala wa kuuza na kuyaunganisha baadhi ya makampuni ya simu kwa Tanesco kusitishiwa huduma kutokana na kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yake kimkataba.

Wakati suala hili likiendelea kushughulikiwa na mamlaka zinazohusika tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, huduma zinaendelea kupatikana kupitia Kampuni ya MAXCOM katika Vituo mbalimbali, ATM za CRDB na NMB, NMB Mobile pamoja na ofisi zote za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) nchi nzima hadi siku ya Jumamosi na Jumapili na siku za Sikukukuu kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.