Mhe.
Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Rais
Kikwete akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo
pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi kuwathamini Watanzania
waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya
maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora.
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)
Wakuu
wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete ambaye haonekani pichani.
Waziri
Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula huku Balozi
Sefue akisikiliza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi
wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.
Mhe. Rais Kikwete akiwa ameongozana na Balozi Mulamula kuelekea eneo la kupata picha ya pamoja.
Mhe.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
(Picha na Reginald Philip)