Waziri Mkuu Mstaafu na mtangaza
nia ya kuwania urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono
wana-CCM na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
WAZIRI Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka
na swala la kukatwa jina lake katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi(CCM),
kwani anaamini chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa
mgombea urais wa Tanzania.
Lowassa ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM
na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo,
wakati akitoa shukrani baada ya kudhaminwai na wana-CCM zaidi ya elfu
52.
"Nimekuwa mwana-CCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu,
sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea
atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo
anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? Anakata kufanya hivyo kwa
sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo
msiwe na wasiwasi jina litarudi tu," alisema Lowassa.
Lowassa aliwasili mkoani Ruvuma mapema mchana jana akitokea mkoani
Iringa kwa ajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais
kwa tiketi ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na
kupelekea kufunga barabara kuu ya mjini na akalazimika kupanda juu ya
kibambaza cha jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza hao.
Lowassa, akizungumza na
wananchi wa Mkoa wa Ruvuma waliokuwa wamesimama nje ya Ofisi za CCM za
mkoa huo mjini Songea Juni 21, 2015, alipofikuchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25, 2015.
Lowassa
akisalimiana na Chifu wa Wangoni, Chifu Ally Yussuf Songea (97). Chifu
huyo alikwendwa kwenye uwanja wa ndege wa Songea kumpokea Mh. Lowassa.
Kinamama wa Ruvuma wakimshangilia Lowassa.
Mmoja wa wazee wa Ruvuma, Ally Jaibu Rashid, akitoa neno kwa niaba ya wazee wenzake.
Lowassa akizungumza machache na wazee waRuvuma.
chanzo GPL