Chama cha upinzani nchini Afrika ya
Kusini kimetaka uchunguzi kufanywa nchini humo kufuatia hatua ya
serikali kushindwa kumkamata rais wa Sudan Omar el Bashir ambaye
ameshtakiwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika mahakama ya ICC.
Bwana
Bashir alikuwa nchini Afrika kusini wiki iliopita kwa mkutano wa
viongozi wa Afrika lakini alikaidi agizo la mahakama la kumtaka asalie
nchini humo.Chama cha muungano wa Kidemokrasia kimesema kuwa kinataka kujua ni nani aliyemruhusu bwana Bashir kuondoka nchini humo.
Kinasema kuwa serikali ilihusika katika mpango wa kumsaidia kuondoka nchini humo.