Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi akiongea na Maafisa Vijana
waliohudhuria Mfunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu kutumia elimu na uzoefu
watakaoupata katika mafunzo hayo kuwainua vijana kiuchumi kwa kutoa
elimu itakayowajenga na kuwafanya vijana kujitegemea na kuwa
wajasiriamali, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Arusha.
Kulia ni Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi
cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) Bw. Leon
Malisa.
Baadhi
ya Maafisa Vijana wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James
Kajugusi wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Maafisa
Vijana Nchini wametakiwa kutumia elimu wanayopata katika kuwaendeleza
vijana kiuchumi ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za uzalishaji
mali.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James
Kajugusi wakati wa Ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mafunzo ya
Ujasiriamali na ubunifu.
Bw.
Kajugusi alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwaendeleza vijana nchini
Wizara kwa Kushirikiana na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa
Afrika (ESAMI) wameanzisha mradi unaolenga kuwawezesha vijana
kijasiriamali nakiubunifu kwa kupitia mafunzo wanayowapa Maafisa Vijana.
“tunawaomba
kushiriki kikamilifu katika mafunzo haya ya ujasiriamali na ubunifu kwa
kuwasikiliza wawezeshaji kwa makini kwa dhumuni la kutumia elimu hiyo
kuwainua vijana nchini kiuchumi na kuwawezesha kushiriki kikamilifu
katika ujasiriamali”. Alisema Kajugusi.
Naye
Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha
Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Bw. Leon Malisa alisema kuwa
dhumuni la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Maafisa Vijana katika eneo
la ujasiriamali na ubunifu ili kuwawezesha kuitumia Elimu hiyo kwa
vijana vijana nchini kwa kuwawezesha kujiajiri wenyewe.
Aidha
Bw. Malisa ametaka vijana nchini kuunda vikundi na kubuni miradi
itakayowaendeleza ili Wizara kwa kushirikiana na ESAMI waweze kuwasaidia
kujiendeleza ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na tatizo la Ajira
Nchini.
Akizungumzia
kuhusu mafunzo hayo Afisa Vijana toka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bw. Eliackim Mtawa alisema kuwa watatumia mafunzo
haya kuwatayarisha vijana kuwa wajasiriamali wazuri na kuwasimamia
katika utekelezaji wa Miradi hiyo ili kuwawezesha kushiriki katika
uzalishaji mali na kukuza uchumi kupitia ujasiriamali.
Mafuzno
hayo ya Ujasiriamali na Ubunifu yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha
Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI)