Vijana mkoani Mtwara wametakiwa kutumia
fursa za uwepo wa nishati ya mafuta na gesi katika kukuza biashara zao
na uchumi wa mkoa huo.Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo
ya ujasiriamali mkoani humo, baadhi ya vijana hao wamesema kuwa fursa
zilzizopo mkoani humo ni lazima ziwanufaishe vijana ili waendane na
ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.
Kampuni ya Airtel Tanzania, kupitia mradi wake wa “Airtel Fursa
Tunakuwezesha” imewapatia mafunzo na kuwawezesha mitaji baadhi ya vijana
wa manispaa ya mtwara kwa lengo la kuwawezesha kumudu uendeshaji
biashara zao na kukuza mitaji yao.Idd Abdallah ni mjasiriamali aliyenufaika na mafunzo hayo ambaye anasema kuwa kwa sasa amepata muongozo mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi.
“Hii ni fursa ya kipekee kwangu kama kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu na vijana wenzangu wa hapa mtwara” Alisema Abdallah.
Nae mkuu wa wilaya ya Mtwara bi.Fatuma Ally, alisema “mafunzo haya yatapanua wigo wa ufahamu kwa vijana hawa ambapo aliwataka kujituma kwani fursa zipo nyingi mkoani humo.“Mtwara kuna maeneo mengi sana yenye fursa kwa vijana kujiendeleza hivyo nawataka vijana kutumia fursa na mafunzo haya kuhakikisha wanajiendeleza kiuchumi” alisema mkuu huyo wa wilaya.
Hawa Bayumi ni Meneja Maendeleo ya Jamii wa Airtel, alisema hiyo ni fursa inatolewa na Airtel kwa lengo la kusaidia vijana kupata fursa ya kujiajiri na kupata mitaji kupitia mpango huo.“Kwetu sisi Airtel tunaona ni fahari kuwawezesha wajasiriamali kwa mafunzo na mitaji ili waweze kuendeleza biashara zao na kukuza mitaji pia. Alisema Bayumi.
Ugunduzi wa gesi na mafuta mkoani hapa, vijana wanapaswa kujituma kwa kuongeza elimu na mitaji ili waweze kuwa sehemu ya wanufaika na kuondoka na hali ya kuwa watazamani wa tunu hiyo.