Lowassa akiwa Makao Makuu ya CUF jana.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekanusha taarifa za
kupiga marufuku maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu mgombea Urais
wa Chadema, Edward Lowassa.Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa maandamano wanayoyatambua ni yanayoanzia Makao Makuu ya Chadema kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), lakini ya kutoka NEC kwenda Makao Makuu ya Chama Cha Wananchi (CUF), Buguruni hawayatambui.