Uokoaji ukiendelea
Mecca, Saudi Arabia
Upepo mkali umeukumba msikiti mkubwa
zaidi dunia wa Masjid al-Haram uliopo katika Mji wa Mecca nchini Saudi
Arabia na kuua watu wapatao 107 huku wengine 238 wakiwa majeruhi.
Tukio hilo lilitokea jana ijumaa majira ya mchana baada ya upepo huo
mkali uliokuwa ukivuma kwa kasi ya ajabu kuikumba kreni ya mizigo
iliyokuwa ikitumika kwa ujenzi juu kabisa ya ghorofa la msikiti wa
Masjid al-Haram.Baada ya upepo kuikumba kreni iliangukia kwenye msikiti hivyo kuporomosha msikiti huo na kusababisha vifo vya watu 107 na maafa mengine zaidi.
Gavana katika Mji wa Mecca ameamrisha kufanyika uchunguzi kufuatia tukio hilo.
Mkuu wa idara ya ulinzi wa angani nchini humo alisema kuwa, kulikuwa na mvua kubwa wakati ajali hiyo ilipotokea na upepo ulikuwa ukivuma kwa mwendokasi wa takriban kilomita 83 kwa saa. Msikiti huo unazunguka eneo takatifu la kiislamu la Kaaba na ndio msikiti mkubwa zaidi duniani na huwavutia mamia ya waislamu ambao huenda kuhiji kila mwaka. Karibu watu milioni moja wamewasili nchini Saudi Arabia kabla ya sherehe za mwaka huu ambazo zinaanza wiki mbili zijazo.
CHANZO: BBC NA CNN