MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Sep 8, 2015

Ruge aelezea kwanini baadhi ya nyimbo hazipigwi Clouds FM


10406473_886902624722996_7312364841864995813_n
Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefafanua kwanini baadhi ya nyimbo za wasanii wa Bongo hazipigwi Clouds FM. Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi TV cha EATV, Ruge alikiri kuwa matatizo hayo yalikuwepo mwanzo lakini kwa sasa wameyatafutia suluhisho kwa kuanzisha idara inayoshughulikia muziki.

“Unajua saa zingine tunachukua hivi vitu ni rahisi. Mtu anachukua CD anapanda nayo juu anacheza, haya matatizo mwanzoni labda ya kuanzisha utaratibu mpya yalikuwepo. Lakini tunavyokua, kumbuka redio yetu ni changa, ndio tuna miaka 16, lakini bado ni changa katika mfumo wa redio kwa sababu mwanzo ulikuwa unakuja na CD unaingia nayo studio, sasa hivi kila kitu kinapigwa kwenye computer,” alisema.
“Nyimbo inapoletwa redioni inasikilizwa na idara nzima ya muziki ili ipitishwe na idara nzima ya muziki. Nyimbo zilizopita zinaandikwa, zilizopita ni hizi na zisizopita ni hizi, ambazo hazijapita ni hizi na watu ambao nyimbo zao hazijapita zinarudishwa chini na kila nyimbo inayorudishwa lazima mtu aandikiwe kwanini nyimbo hii haijapita, ili kama ana nafasi ya kwenda kuirekebisha akarekebishe,” alifafanua Ruge.
“Hakuna nyimbo inayoletwa ikapita tu na mimi naamini nyimbo nzuri ni nzuri tu na mbaya ni mbaya au isiyokuwa sio nzuri kihivyo basi ikaboreshwe mpaka ifike hatua ya kuwa nzuri. Lakini usipokee nyimbo ambayo hautaipiga, usimwitikie mtu aliyeleta pale ukamwambia hii imepita halafu isipigwe.”
“Hakuna msanii yeyote anayeleta nyimbo redioni ikaenda moja kwa moja. Lazima isikilizwe kwenye music department na hata wasanii wengine wakubwa wanalalamika kwa sababu anakuja anampa rafiki yake nyimbo, lakini anapiga siku hiyo hiyo aliyoitambulisha baada ya hapo haitapigwa tena kwa sababu hakuiletwa kwenye utaratibu uliokuwepo,” aliongeza Ruge.
Katika hatua nyingine Ruge alisema ilifikia wakati alitaka kuachana na muziki kutokana na kutukaniwa ndugu na watu wake wa karibu wasiohusika na anachokifanya.
“Mimi hapa nadhani kuna kipindi nilikuwa nusu niache haya masuala ya muziki,” alisema.
“Kwa sababu nikagundua sio mimi inaniathiri, mama yangu anatukanwa, ndugu zangu wanatukanwa, watu ambao hawana makosa wanahusishwa. Kwa mfano partner wangu Joseph hayupo kwenye mfumo huu kabisa, lakini unashangaa kuna mtu anamtukana. Joseph hayupo kwenye uendeshaji wa aina yoyote ule.”
“Nikasema labda mimi niache, nikajiuliza hapana mimi nikiacha kwa sababu ya watu wanne watano wanaotukana, Je, wale watu 50 wanaofaidika na mimi kuendelea kuwepo kwenye hii industry nitakuwa nawafanyia nini? Nitakuwa siwatendei haki. Kuna watu kama akina Barnaba, ambao sasa hivi wanapata maisha kwa sababu ya muziki na siy Barnaba wakati wote anatoa nyimbo zinafanya vizuri. Anatoa hii inafanya vizuri, inayofuata haifanyi vizuri. Kwanini hatumii madawa? Kwahiyo ina maana uogope watu kwamba nyimbo isipofanya vizuri watatumia madawa, Haiwezekani. Mimi kama mtu yoyote anavyofanya kazi, unafanya biashara hii inakubali, ikifanya vibaya basi angalia upande wa pili jinyanyue tena fanya tena.”
“Lakini katika hali ya kawaida, kiukweli mimi sitaacha hata nitukwanwe vipi. Na kwa sababu kuna watu niliwaacha na najua ndio sababu ya kuwaacha ndio wakaingia kwenye madawa. Sasa bahati mbaya Ray C alivyoingia kwenye madawa sikuwa nafanya kazi na Ray C. Lakini Ray C alivyopata matatizo ya madawa anakuja kurudi kwangu tena. Sasa maana yake ni nini? Kwanini uwaache watu waende wapate matatizo halafu mwishoni warudi tena wewe ufanye kazi ya kuja kuwasaidia, sasa maana yake ni nini?” alihoji Ruge.