Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga akisoma hotuba kwa niaba ya
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kwenye maadhimsho ya siku
ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akitoa ujumbe maalum kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Unesco, Irina Bokova kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya
Kimataifa ya Amani Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo
akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani
Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akitoa nasaha zake
kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa
yamefanyika jijini Mwanza.
Jukwaa
kuu la viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku
ya Kimataifa ya Amani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo akiteta jambo na Mgeni
rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
Amani, ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kikundi cha kwaya ya Patimo-Mabatini jijini Mwanza kikitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani ya Qaswida maalum iliyobeba ujumbe wa kutunza 'Amani' ikitolewa.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga akiweka saini kwenye Azimio
maalum la kuenzi Amani lililoandaliwa kwenye maadhimisho hayo huku Mgeni
rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dini mbalimbali
la Amani Tanzania (IRCPT), Rev. Canon Godda (wa pili kulia) wakishuhudia
tukio hilo.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo
(kushoto) na viongozi mbalimbali wa dini wakiendelea kusaini Azimio
hilo.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues akiweka sahihi kama shuhuda katika kupitisha Azimio hilo.
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi naye akiweka saini kama
shuhuda wa kupitisha Azimio hilo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Baraka Konisaga.
Pichani
juu na chini ni makundi ya Viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini,
Viongozi wa Serikali, Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Jeshi la
Polisi na Walemavu waliodhuruia siku ya Kimataifa ya Amani Duniani
ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Shule ya
msingi Nyanza.
Wawakilishi wa vikundi vya vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya Amani Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya msingi Nyanza walikuwa ni miongoni mwa
washiriki wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani duniani.
Meza kuu katika picha ya pamoja.
Washiriki katika picha ya pamoja na meza kuu.