Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono
wananchi kuwaaga baada ya kumaliza kufanya kampeni kwenye Uwanja wa
Sabasaba, wilayani Bunda, Mara jana
Watu wakiwa wamefurika kumsikiliza Dk Magufuli akijinadi katika
Mji wa Nyamswa, Bunda Vijijini ambapo ameahidi kukamilisha ujenzi wa
Barabara ya lami inayotoka Bunda kwenda Nyamuswa hadi Musoma.
Dk Magufuli akihutubia wananchi na kuomba kupigiwa kura siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu
Waendesha Bodaboda wakiwa msikiliza kwa makini Dk Magufuli mjini Bunda
Dk Magufuli akiwanadi wagombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini,
Steven Wassira (kushoto) na Ligora wa Jimbo la Mwibara. Ligora
alimmwagia sifa lukuki Dk Magufuli kuwa ndiye chaguo la Mungu kuiongoza
nchi hii kuliko wagombea wengine 7.
Mgombea ubunge Jimbo la Mwibara, Kangi Ligora akinadiwa na Dk Magufuli
Steven Wassira anayewania Jimbo la Bunda Mjini, akinadiwa kwa wananchi
MMadiwani wa Kata za Jimbo la Bunda Mjini kupitia CCM wakinadiwa kwa wananchi
Wassira hoyeeeeeeeeeeee
Alitekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema, Emmanuel Malima akitangaza
rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na CCM baada ya kukerwa na
kitendo cha Mgombea wao wa Ubunge aliyeshinda kura za maoni kukatwa na
kuwekwa Esther Bulkaya aliyehamia chama hicho kutoka CCM, zaidi ya
wanachama wa Chadema 120 wameamua kukimbia chama hicho
Mmmoja wa wanachama wapya wa CCM walioihama ChademaMjini Bunda
Aliyeshinda kura za maoni za kuwania ubunge kupitia Chadema na kukatwa jina lake akitangaza kuhamia CCM Mjini Bunda
Dk Magufuli akiwaaga wananchi mjini Bunda
Dk Magufuli akishauriana jambo na Jaji mstaafu Joseph Warioba
(katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah
Bulembo katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Nyamswa, Bunda Vijijini
Jaji mstaafu Joseph Warioba akitangaza wasifu wa Mgombea Urais
wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli na kwamba anafaa kuwa rais wa
Tanzania tofauti na wagombea wengine saba. Amesema kuwa sifa alizonazo
zinafanana na za Baba wa Taifa, marehemu Julius Nyerere. Warioba ni
mzaliwa wa Nyamuswa.
Makongoro Nyerere ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya kampeni ya CCM,
akimuombea kura Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Nyamuswa
Wananchi wakikubali kumpigia kura zote Dk Magufuli pamoja na Mbunge na madiwa wa chama hicho
Dk. Magufuli ameahidi kujenga barabara za lami na kutatua
taitizo la maji wilayani humo, atakaposhinda urais Oktoba 25 mwaka huu.