Mkufunzi
kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tanga, Hassani Juma Hassani
akitoa mada wakati wa semina ya Airtel Fursa ilivyofanyika hivi karibuni
kwenye ukumbi wa YDCP mkoani Tanga.
Meneja
mauzo wa Airtel Mkoa wa Tanga, Aluta Kweka akizungumza na wauzaji wa
bidhaa za kampuni hiyo wakati wa semina ya Airtel Fursa ilivyofanyika
hivi karibuni kwenye ukumbi wa YDCP mkoani Tanga Meneja
mauzo wa Airtel Mkoa wa Tanga,Aluta Kweka akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu semina ya Airtel Fursa iliyofanyika kwenye ukumbi wa YDCP
mkoani Tanga.
Wafanyabishara wadogo na wa kati zaidi
ya 300 waliopo katika wilaya mbali mbali mkoani Tanga wameongezewa ujuzi
wa elimu ya biashara ili waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi na
kuweza kuongezaza kipato chao na kuchangia pato la taifa.
Kampuni ya Airtel Tanzania, kupitia mpango wake wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha” imewapatia
mafunzo ya ujasiriamali vijana wa manispaa ya Tanga kwa lengo la
kuwawezesha kuboresha uendeshaji biashara na kukuza mitaji yao katika
warsha iliyofanyika katika ukumbi wa YDCP uliopo mkoani hapo.
Akifungua warsha hiyo, meneja mauzo wa
Airtel mkoa wa Tanga Aluta Kweka katika alisema, “lengo letu hasa ni
kuwapatia ujuzi vijana wajasiriamali wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi
24 ili waweze kufanya biashara kwa tija badala ya kufanya kwa mazoea.
Mafunzo haya tunataraji yataongeza tija ya kibiasha ku kuwawezesha
Vijana hawa kujenga ajira kwa vijana wengine huku wakichochea
upatikanaji wa bidhaa na huduma katika jamii inayowazunguka.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya
wajasiriamali waliohudhuria warsha hiyo wameishukuru Airtel kwa mchakato
huo na wameiomba Airtel kuendelea na zoezi hilo kwa wafanyabishara nchi
nzima ili waweze kufahamu umuhimu wa kufanya biashara kwa malengo
zaidi.
Aisha Mtangi ni mfanyabiashara mdogo
anayejihusisha na biashara ya kuuza matunda aliyenufaika na mafunzo hayo
ambaye alisema, “kuwa kwa sasa amepata muongozo mzuri utakaokuza
biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi”
“Hii ni fursa ya kipekee kwangu kama
kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu na
vijana wenzangu wa hapa Tanga” Alisema Aisha.
Airtel imejipanga kufikia mikoa 10 kote
Tanzania hadi kufikia December mwaka huu. Vijana wa mikoa hii
watanufaika na mafunzo ya Ujasiriamali na vitendeakazi kwaajili ya
kukuza biashara zao.