Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akifunga Mafunzo
ya siku mbili ya Waandishi wa Habari za Mahakama yaliyofanyika jijini Dar es
salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akitoa ufafanuzi
kuhusu Kichwa cha Habari ya Mahakamani kilichoandikwa bila kuzingatia Weledi na
moja ya Gazeti la Kila siku wakati wa
mafunzo ya siku mbili ya Waandishi wa
Habari za Mahakama yaliyofanyika jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.
Na. Aron
Msigwa –MAELEZO.
27/11/2015.Dar
es salaam.
Mahakama
ya Tanzania imesema kuwa itendelea kufanya kazi na vyombo vya Habari nchini katika
kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa jukumu la Kikatiba ililonalo la kutafsiri
sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi ili kuwawezesha wananchi kujua na kupata
Haki zao kwa wakati.
Akifunga
Mafunzo ya siku 2 ya waandishi wa Habari za Mahakama jana jijini Dar es salaam Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila aliwataka waandishi hao kutimiza
wajibu wao wa kuueleza umma taarifa sahihi za mashauri mbalimbali yanayotokea
mahakamani kwa kuzingatia sheria.
Alisema
vyombo vya habari na mahakama vinahitajiana, vinafanya kazi pamoja kwa manufaa
ya umma huku akieleza kuwa mikutano ya mara kwa mara kati ya wanahabari na
mahakama kunaongeza kuaminiana na kujenga mahusiano mazuri.