Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mtume TB Joshua wa kanisa la Church
of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
Picha na Freddy Maro.
Dkt Magufuli ampokea TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa
Dkt Magufuli ampokea TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa
Mtume
TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria ametua
jijini Dar es salaam leo tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa
Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara
tu baada ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB
Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho
Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa
uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB
Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi
wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na
Fanaka tele katika awamu hii mpya.