MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Nov 2, 2015

MMILIKI WA FM ACADEMIA AFARIKI DUNIA

Martin Kasyanju enzi za uhai wake.
Mmiliki wa Bendi ya FM Academia, Martin Kasyanju amefariki dunia jana akiwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.
Msemaji wa Bendi ya FM Academia, Kelvin Mkinga amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kusema kuwa Martin amefariki akiwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa takribani wiki mbili.
Kwa mujibu wa Kelvin ni kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria lakini baadaye ikagundulika kuwa ana ‘Pneumonia’ (Nimonia).
Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Mahenge, Oysterbay jijini Dar na mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.