JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA
TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
amemteua Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kipindi cha miaka
miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Oktoba 2015.
Uteuzi
huo ni kwa mujibu wa kifungu Na. 9 (4) (a) cha Sheria Na. 20 ya Mwaka
1993 iliyoanzisha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Prof. Tolly Salvatory
Augustin Mbwette amekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa
kipindi cha miaka kumi kuanzia tarehe 13 Aprili 2005 hadi tarehe 13
Aprili 2015. Pia amekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa
taaluma ni Mhandisi ujenzi aliyobobea kwenye maeneo ya Mazingiria,
TEHAMA, Utawala na Menejimenti kwa zaidi ya miaka 25 na amesoma Vyuo
Vikuu vya Dar es Salaam, Tanzania; IHE Delft, Netherland; na Chuo Kikuu
cha London, Uingereza kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na
Uzamivu. Pia ameshirikiana na Vyuo Vikuu mbali mbali duniani kutoka Bara
la Ulaya, Amerika, Asia na Afrika katika maeneo ya uhandisi, utafiti,
TEHAMA, uandishi wa vitabu na majarida mbali mbali.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia